Hafla ya kuapishwa kwa mawaziri Kaunti ya Taita Taveta. [Picha/ Eddie Nyange]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mawaziri saba wa Kaunti ya Taita Taveta waliapishwa siku ya Jumanne kwenye hafla iliyofanyika katika afisi ya gavana huko Wundanyi.Mawaziri hao ambao waliidhinishwa na bunge la kaunti ni Claris Mnyambo wa Ardhi na Mazingira, Bigvai Mwailemi ambaye sasa atasimamia idara ya Vijana, michezo na masuala ya kijamii, Getrude Nawoti atakaye ongoza idara ya Biashara na utalii na Davis Mwangoma wa Kilimo, mifugo na uvuvi.Wengine ni Dkt Frank Mwangemi ambaye sasa ndiye atakayeongoza sekta ya afya katika kaunti ya Taita Taveta, Daniel Makoko Mwakisha ambaye atasimamia idara ya elimu na Dkt Vincent Masawi ambaye atasimamia sekta ya fedha na mipango.Akizungumza katika hafla huyo, Gavana wa Kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja amewataka wafanyakazi wa serikali ya kaunti kuwajibika ipasavyo katika kazi zao ili kuhakikisha kaunti inasonga mbele kimaendeleo.“Kuna haja ya wafanyakazi kujitolea kikamilifu kuhakikisha wanawahudumia wananchi ipasavyo,” alisema Samboja.Matamshi yake yaliungwa mkono na Naibu Gavana Majala Mlagui ambaye amelitaka baraza hilo jipya la mawaziri kuweka agenda ya mwananchi mbele kwa kuzingatia maadili mema.Mlagui alisema kuwa kwa ushirikiano na afisi ya gavana, watahakikisha wamefanikisha ugatuzi.Kwa upande wake, Spika wa Taita Taveta Meshack Maghanga alisema kuwa ipo haja ya kuwepo kwa vikao vya mara kwa mara kati ya baraza hilo na bunge la kaunti ili kuwezesha ulainifu wa utendaji kazi.Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi tofauti akiwemo Kamishna wa Taita Taveta Kula Hache.