Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mombasa mwaka huu imekuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa mawaziri wa fedha kutoka mataifa ya kanda ya Afrika mashariki.

Mkutano huo wa pamoja ulioanza Jumamosi unatarajiwa kujadili kwa kina changamoto za kiuchumi zinazokumba nchi hizo.

Watakaojumuishwa katika kongamano hilo pia ni pamoja na makamishna wakuu wa forodha kutoka Kenya, Uganda na Rwanda.

Akizungumza mjini humo, kamishna mkuu wa mamlaka ya KRA John Njiraini alisema kuwa wamepokea habari kwamba kuna ulaghai unaofanyika ambapo mizigo iliyobebwa na trela inaelekezwa sehemu zingine.

“Kenya inafanya kazi kwa pamopa na mataifa jirani kukabili tatizo hilo, na hii ndio sababu mojawapo ya kufanya mkutano huu.” Alisema Njiraini.

Aidha kamishna huyo anayewakilisha Kenya pia ameongeza kuwa mkutano huo unatarajiwa kuleta suluhu ya changamoto zinazoshuhudiwa katika biashara hiyo.