Serikali ya Kaunti ya Kisii imeanzisha mazungumzo na wafanyibiashara kuhusu nyongeza ya ushuru iliyoongezwa na kaunti hiyo.
Akiongea na wanahabari hii leo katika mkahawa wa Gesonso kulipo andaliwa kikao cha wasimamizi wa wanabiashara na walalamishi wengine, Gavana wa kaunti ya Kisii amesema kuwa wameanzisha mazungumzo hayo ili kupata jibu mwafaka na wanabiashara kuhusu msaada uliopitishwa na bunge la kaunti ya Kisii kwa wananabiashara kutozwa kodi mpya ambayo ilikuwa ya juu zaidi.
Gavana Ongwae amesema kuwa watashirikiana na wanabiashara hao ili kuongea na kupata suluu mwafaka na kutatua shida hiyo inayowakumba wanabiashara hao katika kaunti ya Kisii hasa kiwango cha ushuru kilichopitishwa.
Kwa upande wa wanabiashara kupitia mwenyekiti wao Walter Nyakundi amesema wako tayari kufanya mazungumzo hayo na wasimamizi wa Kaunti ili kupata suluu na biashara ziweze kunawiri.
“Tumekubali kufanya mazungumzo na serikali baada ya kuweka kiwango cha juu cha ushuru ambacho kilitufanya kuenda mahakamani,” alihoji Nyakundi.
Mazungumzo hayo yamefikiwa baada ya Mahakama ya Kisii kutoa nafsi kwa pande mbili kufanya mazungumzo nje ya korti na kupata suluu mwafaka.
Samwel Omwando ambaye ni mmoja wa walalamishi amesema wako tayari kuwa na mazungumzo hayo ambayo yalianza hii leo ili wapate jibu mwafaka.
“Hii leo tumeanza mazungumzo na wazimamizi hawa wa Kaunti ya Kisii ili kupata suluhu kwa kodi ya ushuru waliyowekewa ambayo ilikuwa ya juu,” alisema omwando.
Omwando pia aliongezea kuwa kati ya mambo watakayozungumuzia ni kodi,Kuharakishwa kwa wanabiashara,na wanainchi kutochangia katika miswaada mbalimbali ambayo imepitizwa.