Mgombea wa kiti cha ubunge eneo la Kisauni Ali Mbogo amewasuta viongozi wenye tabia ya kusitisha miradi ya kimaendeleo kwa misingi ya kisiasa.
Mbogo aliwakashifu baadhi ya viongozi aliosema kuwa wana tabia ya kujihusisha na propaganda za kuzuia miradi ya kimaendeleo na hata kuwapotosha wananchi katika misingi ya kisiasa, jambo alilosema linawavunja moyo wakaazi wa Mombasa.Akizungumza katika eneo la Kisauni, Mbogo alisema kuwa tabia ya viongozi kuzuia miradi ya maendeleo sharti ikomeshwe mara moja.“Hatua kali za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya viongozi kama hao kwani hatua hiyo imechangia pakubwa wananchi kupitia maisha magumu na hata kukosa huduma bora za kimaendeleo hususan katika sehemu za mashinani,” alisema Mbogo.Mbogo aidha alisema kuwa kuna haja ya viongozi kushirikiana katika maswala ya uongozi badala ya kutengana katika misingi ya kisiasa kama njia moja ya kuhakikisha wananchi wanafaidika na miradi mbali mbali ya maendeleo.Vile vile, aliwahimiza wakaazi wa Mombasa kuwa makini msimu huu wa uchaguzi mkuu na kuwaondoa mamlakani viongozi wabinafsi.