Mgombea wa kiti cha ubunge eneo la Kisauni Ali Mbogo amedai kuwa kuna njama ya kumpokonya tiketi ya chama cha ODM wakati wa uchaguzi wa 2017.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza kwenye kikao na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Mbongo alidai kwamba kuna baadhi ya viongozi katika chama hicho wanaojaribu kumsambaratisha kisiasa.

Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na hali yake ya kujisimamia kibinafsi katika maswala ya kupigania kiti hicho.

“Kamwe sitatishwa na misukosuko ya kisiasa na uvumi unaoenezwa na baadhi ya viongozi wa ODM. Nina uhakika nitashinda wakati wa mchujo,”alisema Mbogo.

Hatahivyo, Mbogo alisema kuwa iwapo hakutafanywa mabadiliko katika chama hicho, basi huenda akajiondoa kutoka chama cha ODM na kuhamia chama kingine katika mrengo wa Cord.