Mwaniaji wa ubunge Kisauni Ali Mbogo katika hafla ya awali. [Picha/ thecoastocunties.com]
Mgombea wa kiti cha ubunge Kisauni Ali Mbogo amepewa cheti rasmi cha kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha Wiper.
Mbogo atamenyana na mbunge wa sasa wa Kisauni, Rashid Bedzimba, ambaye ana ushawishi mkubwa eneo hilo.Akihutubia wanahabari baada ya kupewa cheti hicho na Tume ya IEBC, Mbogo alisema kuwa yuko na matumaini ya kushinda kiti hicho na kumbwaga Bedzimba.“Nina Imani kuwa nitaibuka mshindi kwa sababu wananchi wamechoka na uongozi wa Bedzimba,” alisema Mbogo.Mbogo alimtaja Bedzimba kama kiongozi asiyekuwa na malengo ya kufanikisha mahitaji ya wananchi wa Kisauni hasa katika maswala ya elimu na ajira.“Maswala ya elimu na ajira yamesahaulika hapa Kisauni kana kwamba hakuna mbunge,” alisema Mbogo.Wakati huo huo, Mbogo amewasihi wanasiasa wenzake pamoja na wafuasi wao kufanya kampeni za amani ili kuepuka machafuko.