Mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Mombasa amesema kuwa muungano wa Cord utaendeleza maandamano yake ya kushinikiza kubanduliwa kwa Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Mishi Mboko alidai kuwa tume hiyo imeshindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na inapaswa kuondolewa mamlakani.

Mboko alisema kuwa maandamano hayo ni ya kikatiba na yanaashiria kuwa Wakenya wengi wanatilia dosari tume hiyo.

Kiongozi huyo hata hivyo alikanusha madai kwamba maandamano hayo yanalenga kuutafutia mrengo wa Cordna kinara wake mkuu Raila Odinga umaarufu wa kisiasa.

Mwakilishi huyo wa wanawake alishikilia kwamba maandamano hayo ni ya kupigania uchaguzi ulio wazi na wa haki.

"Sisi kama viongozi wa Cord tutahakikisha tunapigania haki za Wakenya bila uoga hadi maswala muhimu kuangaziwa ikiwa ni pamoja na kusitisha udhalilishaji wa Wakenya wanyonge,” alisema Mboko.