Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nakuru ameipongeza wizara ya ugatuzi kwa kutoa chakula cha msaada kuwasaidia wakazi wa Nakuru.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbugua amekua akisambaza chakula hicho kwa wazee, walemavu na wasiojiweza katika wadi zote za kauti ya Nakuru.

"Chakula cha mahindi, maharagwe, mchele na mafuta kimewafikia wote wasiojiweza, wazee na walemavu, ningependa kushukuru wizara ya ugatuzi kwa kufanikisha mradi huu wa kipekee. Nishukuru wizara hii kwa kukubali wito wangu wa kusambaza chakula hiki kwa wanaokihitaji," alisema Mbugua.

Awali, Mbugua alikumbwa na tuhuma za kuuza chakula cha msaada lakini alitupilia mbali tuhuma hizo kama propaganda