Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nakuru Mary Mbugua ameusuta mrengo wa upinzani CORD kwa kutumia maandamano kushinikiza kubanduliwa kwa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbugua alisema kuwa kuna njia mwafaka za kisheria zinazoweza kutumiwa kuitisha kuondolewa kwa tume hio.

"Ni mbaya kwa CORD kutumia maandamano kuitisha kuondolewa kwa tume ya kikatiba ila kuna njia mwafaka kupitia bunge au mahakama," alisema Mbugua.

"CORD wanafaa kuangalia usalama wa nchi wanapofanya maandamano na watumie njia za kisheria kuibandua IEBC," aliongeza.

CORD ilifanya maandamano Jumatatu katika ofisi za IEBC jijini Nairobi lakini polisi walisitisha maandamano haya kwa kuwatawacha kutumia gesi ya machozi.