Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua amewataka wahudumu wa pikipiki kuheshimu sheria za trafiki ili kuepuka ajali za kila mara.
Akizungumza Ijumaa alipokutana na vikundi mbalimbali vya wahudumu hao Nakuru, Mbugua alisema kuwa ajali nyingi zinazohusisha wahudumu WA pikipiki zinaeza kuepukwa iwapo wahudumu hao watazingatia sheria za trafiki.
"Ajali nyingi za pikipiki nI kutokana na hatua ya sheria kutofuatwa,"alisema Mbugua.
Hata hivyo aliwapongeza wahudumu hao kwa mchango wao katika sekta ya uchukuzi katika kaunti ya Nakuru.
Aliongeza kuwa serikali yake itazidi kuzingatia maslahi ya wahudumu hao ikiwemo ujenzi wa vibanda kuwakinga na jua Kali.
Wakati huo huo, aliwataka kuheshimu kazi yao katika sekta ya uchukuzi na kuepuka kujihusisha na siasa potovu na makundi ya uhalifu.