Gavana wa kaunti ya Nakuru, Kinuthia Mbugua, ametoa hakikisho kuwa viongozi wote wa kisiasa na wa kimikoa katika kaunti ya Nakuru, watafanya mkutano katika eneo la Kosovo mjini Naivasha ili kusuluhisha mizozo ambayo imekuwa ikishuihudiwa katika eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbugu aliyasema haya siku ya Jumatano alipoizuru hospitali ya wilaya ya Naivasha na kukutana na waombolezaji kutoka eneo hilo ambao walipompoteza mpendwa wao baada yake kuuawa kasha kuteketezwa na watu wanaodaiwa kutoka jamii moja.

Mbugua amesema ili kuleta suluhu la kudumu katika mizozo ya ardhi na mipaka katika maeneo mengi ya Naivasha, kuna haja kwa washikadau wote kushirikishwa kwenye mkutano huo ili kuleta mtagusano miongoni mwa jamii za eneo hilo.

“Ningetaka kuhimiza vyombo vya usalama pia kuhakikisha kuwa wanachukua hatua ya haraka kuhakikisha waliotekeleza mauaji ya kijana huyu wanakamatwa na kufunguliwa mashataka mara moja,” aliongeza Mbugua.

Itakumbukwa kuwa maeneo mengi ya kaunti ndogo ya Naivasha, imekuwa ikukumbwa na mizozo ya ardhi, jambo ambalo limepelekea maafa ya watu kadhaa na hata wengine kupoteza mali.