Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua amempongeza rais Uhuru Kenyatta kwa kuruhusu sherehe za kitaifa za Madaraka kuandaliwa Nakuru. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza Jumamosi na wanahabari ugani Afraha baada ya kutathmini shughuli za matayarisho, Mbugua alisema kuwa serikali ya kaunti ya Nakuru inashirikiana na ile ya kitaifa kuhakikisha ufanisi. 

Wakati huo huo, Mbugua alitoa wito kwa wakaazi kuhakikisha wanatumia fursa hiyo vyema. 

"Langu ni kumpongeza tu rais wetu kwa kuchagua Nakuru katika maadhimisho haya na kuwarai wakaazi kutumia fursa hii hasua wafanyibiashara,"alisema Mbugua.

Aliongeza kuwa kando na uzalendo, sherehe hizo kuandaliwa Nakuru ni hatua mwafaka na wafanyibiashara wanafaa kutumia fursa hiyo kujiimaarisha. 

Kuhusu maandalizi, Gavana Mbugua alidokeza kuwa kamati andalizi inajizatiti kila iwezavyo ili kuhakikisha kuwa sherehe hizo zinafana. 

Itakumbukwa kuwa rais Uhuru alipozuru Nakuru mwezi Aprili, alitangaza kurejea mwezi Juni katika sherehe za Madaraka. 

Kwa kawaida, sherehe za kitaifa ikiwemo Madaraka, huandaliwa jijini Nairobi lakini serikali ya Jubilee iliamua kuwa zitaandaliwa katika miji mikuu kwa mzunguko.