Mbunge wa Kisauni.Ali Mbogo katika hafla ya awali. [Photo/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo amewataka vijana wanaojihusisha na kundi la uhalifu la Wakali Kwanza kujitokeza ili wapate elimu itakayo wawezesha kujiendeleza kimaisha.Mbogo amesema kuwa analenga kuangamiza kundi hilo katika eneo la Kisauni, kwa kufadhili elimu ya vijana ambao hawana uwezo wa kulipa karo.Akizungumza katika eneo la Msambweni siku ya Jumatatu, Mbogo alisema ameanzisha mradi wa ‘Elimu Kwanza na sio Wakali Kwanza” unaonuia kuwashawishi vijana hao kuasi kundi hilo la uhalifu.“Ninanuia kuanzisha mradi wa Elimu Kwanza ili kuangamiza kundi hatari la Wakali Kwanza,” alisema Mbogo.Mbogo alisema kuwa mradi huo wa elimu unalenga kuangamiza kundi hilo la uhalifu, ili vijana waweze kupata elimu badala ya kuzurura mitaani wakitekeleza visa vya uhalifu.“Mradi wa Elimu Kwanza unalenga kuangamiza kundi la Wakali Kwanza kwa sababu vijana watapata elimu na hawata fikiria tena kujiunga na kundi hilo la ujambazi,” alisema Mbogo.Mbunge huyo alisema kwamba ni jambo la kusikitisha kuwa kundi hilo la Wakali Kwanza limewahangaisha wenyeji kwa muda mrefu kwa kutekeleza visa vya kihalifu dhidi yao.Aidha, ameitaka idara ya usalama kukaza kamba katika kukabiliana na kundi hilo ili wananchi waweze kuishi kwa amani.“Polisi wanafaa kujitahidi vilivyo ili kundi la Wakali Kwanza liweze kuangamizwa kabisa,” alisema Mbogo.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6