Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi ameikashifu tume ya ardhi nchini kwa kutowafidia wakaazi wa eneo hilo walioathirika kwa ujenzi wa bara bara kuu ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa Moi kupitia kwa mashamba yao.
Aidha mbunge huyo amesema kuwa wameipa tume hiyo makataa ya siku 30 ili kuweka mikakati ya kuwafidia watu au ama waende mahakamani ili kusimamisha ujenzi wa barabara hiyo.
Mwinyi alisema haya siku ya Alhamisi alipokuwa akiwahutubia wakaazi wa eneo hilo walioandaa maandamano ya mani ili kulalamikia kutolipwa na tume hiyo.
Hata hivyo mwenye kiti wa tume ya ardhi nchini Mohammed Swazuri amewahakikishia wakaazi hao wa Changamwe kuwa kila mmoja wao atafidiwa.