Mbunge wa eneo bunge la Bomachoge Borabu Joel Onyancha amehimizwa kuhakikisha barabara zote ambazo zilizinduliwa na Rais Kenyatta zimeanza kukarabatiwa na kukamilika kwa mda unaofaa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wito huo umetolewa baada ya wakaazi wa eneo hilo kusumbuka kwa mda mrefu kutokana na barabra mbovu wanapeleka mazao sokoni.

Akizungumza siku ya Jumapili katika eneo la Marindi Mwakilishi wa wadi ya Magenche kaunti ya Kisii Timothy Ogugu aliomba Mbunge Onyancha kuhakikisha barabara hizo zimeanza kukarabatiwa na kuwekwa lami ili wakaazi waanze kufaidi huduma zake.

“Naomba Mbunge wetu vile alijaribu na kumleta Rais Uhuru Kenyatta katika eneo bunge hili letu na kuzindua baadhi ya barabara ambazo zitakarabatiwa, naomba ahakikishe ukarabati huo umeanza na kukamilika kwa muda unaofaa,” alisema Ogugu.

Miongoni mwa barabara hizo ni ya Riokindo-Magenche-Mariba-Kenyenya ingine ni ya kutoka eneo la Mariba-Nyagancha–Edaraja.