Mbunge wa eneo bunge la Mugirango Magharibi kaunti ya Nyamira James Gesami amehimizwa kujenga vyoo vya shule ya msingi ya Kianyabao baada ya vyoo hivyo kuanguka na kupelekea wanafunzi kuendelea kusumbuka kwa ukosefu wa vyoo.
Wakizungumza mnamo siku ya Jumatatu katika eneo hilo la Kianyabao wazazi wa shule hiyo wakiongozwa na Jackson Mochama na Paul Mong’are waliomba mbunge wao kusaidia shule hiyo kujenga vyoo hivyo ili wanafunzi kuendelea na masomo yao kama kawaida
“vyoo vya shule vilianguka na hakuna vyoo vinatumika," alisema Mochama.
"Tunaomba mbunge wetu James Gesami asaidie shule hii kwa ujenzi wa vyoo hivyo vipya ili masomo yawe yanaendelea kama kawaida,” alisema Mochama.
Wakati huo huo, wazazi hao waliomba serikali ya kaunti ya Nyamira kwa ushirikiano na wahisani wema kujitokeza kutoa usaidizi kwa shule hiyo ili wanafunzi kurejelea masomo yao.
Baada ya vyoo hivyo kuanguka kanisa la kiadventista ya Kianyabao lililazimika kufungua vyoo vyake ili wanafunzi wa shule hiyo iliyoko karibu na kanisa hilo kutumia wakisubiri vyoo hivyo kutengenezwa
“Ikiwa serikali ya kaunti inahitaji kutusaidia itusaidie sasa kwa maana hatuna pa kuenda ” alisema Mong’are.