Mbunge wa eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira Timothy Bosire amehimizwa kutoa usaidizi kwa shule ambazo vyoo vya wanafunzi vilifagiliwa na mvua.
Wito huo umetolewa baada ya vyoo vya shule ya msingi ya Kiamakondo iliyoko wadi ya Kemera eneo bunge la Kitutu Masaba kufagiliwa na mvua huku walimu na wanafunzi wa shule hiyo wakiachwa bila msala wa kutegemea.
Akizungumza siku ya jumapili alipotembelea shule hiyo ya Kiamakondo mwanasiasa katika eneo bunge hilo Victor Ogeto aliomba mbunge wa eneo hilo kutoa msaada kwa shule hiyo na zingine..
“Mvua ambayo inaendelea kunyesha katika eneo la Kisii imesababisha madhara mengi na baadhi ya vyoo vya shule vimefagiliwa na mvua ninaomba Mbunge Bosire kuingilia kati na kutoa usaidizi ili vyoo vipya vijengwe,” alisema Ogeto.
Aidha, Ogeto aliomba serikali ya kaunti ya Nyamira nayo kuingilia kati kusaidia changamoto zile zinakumba baadhi ya shule katika kaunti hiyo.