Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi katika hafla ya awali. Picha/ the-star.co.ke

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi ameitaka serikali kubuni mikakati itakayo punguza gharama za matibabu katika vituo vya afya nchini, hasa upande wa uchunguzi wa magonjwa mbali mbali.Akizungumza na wanahabari alipopokea dawa za aina tofauti zilizogharimu shilingi 450,000 kutoka kwa mamlaka ya Bandari ya Mombasa, Mwinyi alisema kuwa hatua hiyo itaimarisha huduma za afya humu nchini.Mbunge huyo alidokeza kuwa ni wazi kuwa idadi kubwa ya Wakenya humu nchini hawana uwezo wa kupata huduma bora za afya kwa kuwa gharama za matibabu ziko juu mno.Mwinyi alisema kuwa sharti swala hilo lishughulikiwe kwa haraka kwa manufaa ya mwananchi wa kawaida.Wakati huo huo ameitaka Wizara ya elimu kupunguza viwango vya karo kwa wanafunzi wanaosomea taaluma ya udaktari kwani idadi kubwa ya wanafunzi hao hawana uwezo ya kulipa karo kutokana na hali ngumu ya maisha.