Mbunge wa Nyali Hezron Awiti ameshikilia msimamo wake wa kuwania kiti cha ugavana kupitia chama cha Wiper katika uchaguzi mkuu ujao.
Wiper ni mojawapo wa vyama tanzu vya mrengo wa Cord.
Akiongea katika eneo la Changamwe siku ya Jumanne kwenye mkutano na jamii ya Wakamba katika kiwanda cha Akamba Handcraft, Awiti alipinga vikali madai ya kuhama muungano wa Cord na kujiunga na ule wa Jubilee.
Aidha, mbunge huyo amemtaka Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho kuwajibika kwa kusikiliza vilio vya wananchi wa kawaida.
Awiti alisisitiza kuwa ana vigezo vya kumruhusu kuwa kiongozi na katu hatababaishwa na ukabila.