Mbunge wa Mvita Abduswamad Sharrif amekashifu Naibu Rais William Ruto kwa kusema kuwa Mrengo wa Cord ina nuia kuwagawanya Wakenya kikabila ili kushinda uchaguzi mkuu ujao.
Akiongea mjini Mombasa siku ya Jumapili Bw Sherrif alisema kuwa kama kiongozi wa kitaifu Naibu Rais hafai kutoa matamshi kama hayo ambayo huenda ikiwafanya viongozi wote kuonekana wahuni.
Aidha kiongozi huyo pia amesema kuwa mrengo wa Cord ulikuwa na mikakati ya kuunganisha wakenya wote na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakua.
Mbunge huyo pia alishiilia kuwa lazima tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka uchunguzwe upya kuhusa sakata ya chiken gate na maafisa waliohusika kuchukuliwa hatuaza kisheria.