Wazazi wote wameombwa kushirikiana na waziri wa elimu nchini Fred Matiang'i ili kuinua sekta ya elimu nchini .

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa ushirikiano utafanikisha jitihada za kuhakikisha sekta ya elimu imeinuka.

Kulingangana na mbunge wa eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini Jimmy Angwenyi, kila mzazi akishirikiana na waziri sekta hiyo itainuka zaidi kwani ndio msingi wa maisha kwa kila mwanafunzi.

Angwenyi pia aliomba ushirikiano huo kuwa kati ya walimu na wazazi na washikadau wote wa elimu ili kuboresha sekta hiyo nchini.

“Sisi sote tunastahili kuwa pamoja na kufanya kazi na Waziri Matiang'i ili kuinua sekta ya elimu ambayo ni muhimu zaidi,” alisema Angwenyi.

Wakati huo huo, Angwenyi alisema umoja utaleta mengi katika taifa la Kenya huku akiomba wabunge nao kushirikiana kuleta maendeleo katika jamii ya Kisii kwani maendeleo ndio ya manufaa zaidi kwa wakazai wa jamii ya Gusii