Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amepinga hatua ya serikali kutaka kuhamisha wakaazi wa eneo bunge hilo walio karibu na Uwanja wa ndege wa Moi jijini Mombasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza katika hafla ya kuzindua kaunti ndongo ya Jomvu siku ya Jumatano, mbunge huyo alidai kuwa huenda hiyo ni njama ya mabwenyeye kutaka kunyakua ardhi zilizoko karibu na uwanja wa ndege kwa kuwa wanajua dhamani yao.

Omar alisema kuwa si mara ya kwanza mpango kama huo kutokea kwa kuwa mwaka uliopita, wakaazi wa eneo la Dunga Unuse pia walikabiliwa na changamoto kama hizo ila walitafuta njia ya kuzikabili.

“Wakaazi wa Dunga Unuse walitaka kuhamishwa kwa sababu ya ujenzi wa behewa mpya iliyokuwa ikijengwa bandarini, akini kama viongozi tulihakikisha njia mbadala imepatikana,” alisema Mwinyi.

Mbunge huyo sasa ametoa lawama kwa mshirikishi mkuu wa Usalama katika ukanda wa Pwani Nelson Marwa kwa kuingilia mambo ya Ardhi.