Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir ametoa tahadhari kwa mrengo wa Jubilee kuwa atawasilisha mswada bungeni ili kamati ya bunge kuhusu fedha itathmini jinsi walivyotumia fedha katika uchaguzi mdogo wa Malindi uliokamilika.
Akihutubia mkutano wa wananchi katika eneo la Mvita siku ya Jumapili, mbunge huyo alidai kuwa Mrengo wa JAP ulitumia takriban shilingi milioni 300 katika kuwahonga wakaazi wa Malindi ili waweze kunua kura 9, 000 za wakaazi hao.
Nassir aidha alidai kuwa huenda fedha hizo ni kati ya zile zilizopotea katika sakata ya Eurobond, pamoja na zile ya sakata ya NYS ambazo zinadaiwa kuwa takriban shilingi milioni 791.
“Niko miongoni ya wabunge wanaoketi katika kamati ya bunge inayochunguza fedha zilizopotea na nitahakikisha hela hizo zimechunguzwa,” alisema Nassir.