Mbunge Rashid Bedzimba ameitaka idara ya usalama kuwatia mbaroni walanguzi wakuu wa mihadharati eneo la Magodoroni, gatuzi dogo la Kisauni.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Bedzimba ameelezea wasiwasi kufuatia kukithiri kwa utumizi wa mihadarati miongoni wa vijana katika eneo hilo.

Mbunge huyo alilitaja eneo la Magodoroni kama soko huru la dawa za kulevya.

Akizungumza siku ya Ijumaa, Bedzimba aliwataka polisi kuwakabili vilivyo wanaohusika na uuzaji wa dawa hizo eneo la Kisauni.

Alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona vijana wengi katika eneo hilo wakiwa wameharibika kutokana na utumizi wa mihadarati.

“Itakuwa bora iwapo watu wanaouza dawa za kulevya eneo la Magodoroni watakamatwa na kufukishwa mahakamani,” alisema Bedzimba.

Aidha, alisema kuwa hatua za dharura zinapaswa kuchukuliwa kwani vijana wengi wanaacha shule na kujiunga na biashara hiyo haramu.

Vile vile, Bedzimba aliwataka wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao ili kuwaepusha na utumizi wa dawa zakulevya.