Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga katika hafla ya awali. Picha/ the-star.co.ke

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga ametangaza rasmi kuwa amekihama chama cha KADU Asili na kuunda chama chake kipya cha Devolution Party of Kenya (DPK).Akizungumza katika kikao na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatano, baada ya kukutana na wajumbe kutoka maeneo mbalilimbali ambao tayari wameonyesha ari ya kugombea viti vya kisiasa kupitia chama hicho kipya, Mwinga alisema kwamba aliafikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa baadhi ya wanachama wa KADU Asili wana ubaguzi.Mwinga ambaye alikuwa kinara wa KADU Asili alisema kuwa kwamba chama hicho kipya cha DPK kina sera muhimu za kuhakikisha Wakenya wote katika maeneo ya mashinani wananufaika na miradi ya maendeleo.Hata hivyo, mbunge huyo alidinda kuweka wazi mrengo watakao uunga mkono kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti na kusema kuwa wataandaa kongamano na wagombea wote na kufanya uamuzi wa pamoja.Chama cha DPK kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni.