Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir ameunga mkono pendekezo la Gavana wa Mombasa Hassan Joho la kupitishwa kwa mswada wa ugaidi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza alipohudhuria kongamano la Global Summit nchini Uturuki, Joho alisema kuwa wameweka mikakati ya kukabiliana na ugaidi katika kaunti hiyo.

Swala hilo lilipokelewa vyema na washika dau waliokuwa wamehuthuria kongamano hilo.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Africa lilithibitisha kuwepo kwa mkakati huo wa kukabiliana na vitendo vya ugaidi.

Shirika hilo liliandaa kikao na Mbunge wa Mvita Bwana Abdulswamad Nassir siku ya Jumanne kujadili mkakati huo haswa namna ya kuitekeleza miongoni mwa vijana.

Mbunge huyo alikubali kushirikiana na shirika hilo kukabiliana na janga la ugaidi katika Kaunti ya Mombasa.

"Tunawakaribisha washika dau wote kuungana nasi kuhakikisha swala la ugaidi limekabiliwa katika Kaunti ya Mombasa,” alisema Nassir.

Shirika hilo la Haki Afrika litachukua maoni kutoka washika dau wa usalama kuhusu jinsi mikakati hiyo itakavyotekelezwa.