Mbunge wa eneo bunge la Borabu Kaunti ya Nyamira, Ben Momanyi, amewafadhili wanafunzi kumi kutoka eneo bunge lake godoro,vitabu na vitu vingine vya kutumia shuleni ili kurejelea masomo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wanafunzi hao kumi walipokezwa vitu hivyo siku ya Jumanne katika eneo la Nyasiongo huku wakiambiwa wasome kwa bidii.

Wanafunzi hao wanasoma katika shule ya wavulana ya Cardinal Otunga Mosocho iliyoko eneo bunge la Kitutu Chache kusini, kaunti ya kisii.

Shule hiyo ilikumbwa na mkasa wa moto na kuchoma vitu vya wanafunzi katika bweni tatu ambazo zilichomeka.

Shule hiyo ilirejelea masomo jana baada ya kufungwa kwa majuma mawili yaliyopita.

Wanafunzi hao wa Borabu walifadhiliwa na mbunge wa eneo hilo ili waweze kurejelea masoma yao.

Wanafunzi hao walimshukuru mbunge wao kwa usaidizi huo na kusema wataendelea na masomo yao kama kawaida baada ya vitu zao kuharibika kufuatia mkasa huo wa moto.

“Pole kwa kuathiriwa na mkasa huo wa moto. Nawaomba muendelee na masomo yenu na mfanye bidii ili muweze kujisaidia nyakati zijazo,” alisema Momanyi.

Aidha, mbunge huyo alisema kuwa ataendele na kuwasaidia wanafunzi wale wanatoka familia maskini katika masomo ili wasome na waweze kujisaidia siku za usoni.

“Wale wanafunzi ambao hawajiwezi katika eneo bunge langu nitahakikisha mumesoma na nitawasaidia katika masomo yenu,” alisema Momanyi.