Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amewashtumu baadhi ya wafanyakazi wa umma kwa kujihusisha na sakata za ufisadi na kuchangia kudidmia kwa uchumi wa nchi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumanne, Awiti alisema kuwa ni lazima kwa wafanyakazi wa umma kukoma kujihusisha na ufisadi na badala yake kujenga taifa hili kwa kuekeza zaidi katika uchumi wa nchi.

Awiti ali,sema kuwa iwapo swala hilo la ufisadi halitasitishwa, basi ataungana na Muungano wa wafanyikazi nchini COTU sambamba na wananchi kumshinikiza Rais Uhuru Kenyatta kuwajibikia majukumu yake.

"Ni lazima kwa maafisa wa umma kukoma kujihusisha na ufisadi ndio taifa hili liweze kuimariska kimaendeleo. Iwapo hawata asi tabia hiyo, basi tutamshinikiza rais kuchukua hatua zaidi,” alisema Awiti. 

Mbunge huyo wa Nyali alisema kuwa taifa hili limebarikiwa na raslimali nyingi ambazo zikitumika vyema, zitahakikisha kuwa uchumi umeimarika na nafasi za ajira kwa vijana kubuniwa.