Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amewakashifu viongozi wa Mombasa wenye mazoea ya kubandika mabango na picha zao katika miradi tofauti.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Awiti aliwakosoa wabunge hao kwa kuwapotosha raia kwa kusema kuwa pesa wanazotumia kutekeleza miradi hiyo sio pesa zao binafsi bali ni ushuru unaotozwa wananchi hao.

Akizungumza siku ya Ijumaa katika eneo la Freretown, Awiti alishangazwa na jinsi wanasiasa wanajipatia umaarufu kwa kuweka mabango yenye picha zao kwenye miradi mbalimbali kama njia moja ya kujipigia debe.

Awiti alitoa wito kwa wanasiasa wenye kasumba kama hiyo kukoma kutumia miradi ya raia kujipatia umaarufu.

"Ninapokuwa nikitembea katika mitaa ya Nyali, mimi huona picha za wanasiasa kwa mashule, barabara na miradi mingineo. Hio ni kazi ya pesa zao? Hio ni ushuru tunaolipa na tunapasa tukague miradi hio kamili,” alisema Awiti.

"Yeyote anayeweka sura na jina lake kwa mabango akidai kuwa yeye ndiye aliyefadhili mradi flani ni muongo sana. Hio ni pesa ya mlipa ushuru,” alisema Awiti.