Mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba ameonya kuwa mwanasiasa yeyote ambaye anatofautiana na Gavana wa Mombasa Hassan Joho kisiasa katika kanda ya Pwani ataangushwa na wananchi katika uchaguzi mkuu ujao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bedzimba alisema haya wakati alipokuwa akitoa vyakula vya msaada katika eneo bunge lake siku ya Jumatatu nakusema kuwa Gavana Joho amepigania haki za wakaazi wa Pwani kwa jumla na hivyo hapaswi kupingwa kwa kazi anayoifanya.

Aidha, mbunge huyo pia aliongeza kuwa wakati wa Wapwani wote kuungana kisiasa ilikuwa imefika na kiongozi yeyote ambaye alikuwa na nia ya kuwapotosha wakaazi ni lazima asichaguliwe tena kuongoza Pwani.

“Ikiwa tunataka kutambulika kisiasa kama kanda ya Pwani lazima tumuunge mkono kiongozi mmoja kututetea huko mbele na kiongozi huyo ni Hassan Joho,” alisema Bedzimba.