Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir amewataka vioingozi wa dini kuwa mstari wa mbele katika kuliombea taifa hili hasa wakati huu linapokumbwa na mizozo mbali mbali.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Nassir alisema kuwa nchi hii imekumbwa na changamoto nyingi ikiwemo matamshi ya uchochezi kutoka kwa viongozi.

Akizungumza siku ya Jumapili katika msikiti wa Hairat mjini Kilifi, Nassir alisema kuwa kuna haja ya viongozi na wananchi kuwa na mazingatio mema ili kuepuka fujo na ghasia kama zilizoshuhudiwa mwaka wa 2007.

“Jamani tuweni mstari wa mbele kuiombea nchi hii kwa sababu kuna changamoto nyingi zinalikumba kwa wakati huu,” alisema Nassir.

Wakati huo huo, ameitaka tume ya uwiano na utangamano kuhakikisha kuwa inaangalia vyema hotuba za uchochezi badala ya kuwatia mbaroni viongozi ambao hawana hatia.

Kauli ya mbunge huyo inajiri baada ya baadhi ya viongozi wa Cord na Jubilee kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kutoa matamshi ya chuki.