Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria amewapa changamoto magavana wa muungano wa Jubilee kwa kile alichokitaja kama kutoajibika kwa kazi yao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni kufuatia kuorodesha kwa Benki ya Dunia namna hela za maendeleo zilivyotumika katika majimbo mbalimbali.

Mbunge huyo  aliyeongea na waandishi wa habari mjini Nakuru alisema kuwa hatua ya majimbo mengi kubaki nyuma inatokana na kutoelewana kunakoshuhudiwa kati ya viongozi Magavana pamoja na Maseneta katika mengi ya majimbo nchini.

Gikaria amehoji kuwa sharti kuwe na majadiliano yatakayopelekea kuelewana na hivyo kuimarisha kiwango cha maendeleo nchini kati ya Gavana na Seneta wa Kaunti ya Nakuru akizingatia kuwa wao ni kitovu katika kufanikisha ugatuzi.

Akiguzia mpango wa raisi wa kupeleka vifaa vya afya katika hospitali mbili za rufa katika kila jimbo hatua iliyopingwa na magavana hapo awali, kiongozi huyo amesema kuwa ipo haja mpango huo kufanikishwa huku akiwashtumu magavana kwa kile alichokidai kuwa nia yao mbaya ya kutaka kutwikwa jukumu la kununua vifaa hivyo  ndiposa waweze kuzifuja hela hizo.

Amewataka magavana hao kurekebisha dosari zao ili kuzuia visa vya aina hiyo akisema kuwa kama viongozi wawakilishi wa Jubilee hawatakaa chini na kushuhudia magavana hao wakielekeza majimbo yaliyo chini ya serikali ya Jubilee katika njia isiyo mwafaka.