Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari chache Kaunti ya Kisii Richard Tong’i ameomba serikali kuu kuongeza pesa kwa serikali za ugatuzi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea katika hafla ya kusherehekea siku ya Madaraka katika uwanja wa Gusii stadium mbunge huyo alisema kuna haja ya serikali za kaunti kuongezeawa pesa il maendeleo yafanyike katika mashnani.

“Naomba serikali ya kitaifa iangalie na kuongeza pesa kwa Kaunti ili maendeleo yazidi kufanywa katika sehemu za mashinani,” alisema Richard Tong’i mbunge wa Nyaribari Chache.

Kwa upande mwingine baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hiyo walisema wasipoandamana jibu halisi halitapatikana huku wakisema kila mpango unafanywa na serikali ya kaunti ya Kisii hufanywa  wakati hawajui matamshi ambayo Gavana Ongwae alikanusha na kuwaomba wananchi kuchangia kwa mswada haswa mswada wa  ushuru kabla haujapitishwa katika bunge la kaunti hiyo.

“Unajua wananchi huandamana ndio jambo hilo hushughulikiwa kikamilifu lakini vile gavana wetu amesema sisi kama wananchi kwanzia leo tutakuwa tukihusishwa kabla ya miswada kupitishwa hasa ile inatulenga sisi wananchi wa kawaida tunasema pongezi kwa gavana kwa kuanza kutuhusisha,” alihoji Kevin Obiri mkaazi.