Mbunge wa eneo bunge la Bomachoge Borabu  kaunti ya Kisii Joel Onyancha amewaomba viongonzi wa Kaunti hiyo kushirikiana kuinua viwango vya masomo katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza katika uwanja wa chuo cha Kenyeny kilichoko katika eneo bunge lake wakati maafara wa chuo hicho walikuwa wakifuzu, mbunge huyo alisema aliomba viongonzi kuwa na ushirikiano mwafaka ili kuinua viwango vya masomo.

Wakati huo huo, mbunge huyo alisema  kuna haja ya kuongezwa kwa taasisi  za mafunzo katika Kaunti ya Kisii ili wanafunzi wengi wapokee mafunzo amboyo ni elimu bora  ambayo itawasaidia katika siku zijazo na kujiimarisha na kujiendeleza kimaisha.

“Nitazungumza na waziri wa elimu nchini Jacob Kaimenyi aongeze taasisi za mafunzo katika kaunti ya Kisii haswa kwa eneo hili ili wanafunzi wasome waje kujisaidia siku sijazo,”alisema Joel Onyancha.

Aidha, mbunge huyo alisema chuo hicho kinastahili kuwa na ukuta ili wanafunzi kuhakikishiwa usalama wao ili lolote lisije likatokea kama lile lililotokea katika chuo cha Garissa na kusababisha maafa kwa wanafunzi.

Mbunge huyo aliomba serikali ya Kaunti ya Kisii kushirikiana na serikali kuu kuchunguza mikasa ya moto inayotokea kila kuchao katika shule za Kisii na kusema kuna haja ya uchungunzi kufanywa ili chanzo cha moto katika mashule kichulikane wazi.

“Naomba mikasa ya moto ichunguzwe kwa undani na hayo yatafanywa na serikali kuu pamoja na serikali ya kitaifa na tuambiwe ni nini kinasababisha mikasa ya moto ambayo hupelekea wanafunzi kupoteza vitu zao na kupata hasara kubwa katika shule za Kisii,”aliongezea Onyancha.