Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi katika hafla ya awali. Photo/ softkenya.com

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Licha ya Wizara ya Fedha kutenga kiwango kikubwa cha fedha kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018 kwa upanuzi wa Bandari ya Mombasa, baadhi ya viongozi wa upande wa upinzani wamelalamikia hali duni ya ajira katika bandari hiyo.Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi alisema kuwa anasikitishwa na jinsi bandari hiyo haijatoa nafasi za ajira kwa vijana katika Kaunti ya Mombasa.Mwinyi alisema kuwa hatua hiyo imesababisha hali ngumu ya maisha miongoni mwa wakaazi wa Mombasa na katika ukanda wa Pwani kwa jumla.“Ni jukumu la Halmashauri ya Bandari nchini, KPA kuajiri Wakenya bila kujali kabila wala tabaka kwani hatua ya kuajiri watu kwa misingi ya kikabila huenda ikasababisha changamoto nyingi katika Bandari ya Mombasa kama vile ufisadi utakao lemaza huduma,” alisema Mwinyi.Vile vile, ameitaka serikali kutilia mkazo swala la ajira miongoni mwa vijana hususan katika mashirika na kampuni za umma ili kuhakikisha vijana wanaimarika kimaisha.