Wakili Ezekiel Oira amewauliza wakaazi wa eneo Bunge la Nyaribari Masaba kuwachagua viongozi sio kwa misingi wa kuhongwa, bali sera za mgombea kiti.
Akiongea na Mwandishi wa habari huyu, Wakili Oira ambaye pia aligombea kiti cha Ubunge katika eneo hilo, amemkosoa Mbunge wa sasa wa Nyaribari Masaba Elijah Moindi kwa madai ya utepetevu na uzembe katika majukumu yake.
Wakili Oira pia amemkosoa Mbunge Moindi kwa kupendelea sehemu fulani dhidi ya zingine wakati wa kugawa fedha za ustawi wa maeneo Bunge al maarufu CDF.
Wakili huyo vile vile amemsuta Mbunge huyo kuwa anajifunika ngozi ya kondoo ilhali vitendo vyake havyiambatani na maadili ya Mkristu.
"Wengi wenu mnanung'unikia uongozi ulioko lakini makosa ni yenu. Mliyemchagua ana ubinafsi mwingi na pia ana ubaguzi na mapendeleo katika kugawa CDF ambapo ni baadhi tu ya Shule na sehemu zinazonufaika na mpango huo wa Serikali ya kitaifa," alisdai Wakili Oira.
Hata hivyo Oira amewashauri wapiga kura kuwachagua viongozi wenye maono thabiti kwa sehemu wanazoziwakilisha.
Wakati mwingine, Oira amedokeza kuwa atagombea kiti hicho cha Ubunge kwa mara ya pili itakapotimu mwaka wa 2017.