Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir katika hafla ya awali. [Picha/ kenyans.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameahidi kushirikiana zaidi na Gavana wa Mombasa Hassan Joho kupiga vita dhulma zinazotekelezwa na serikali ya Jubilee kwa wakaazi wa Mombasa.

Akizungumza siku ya Alhamisi wakati wa sherehe za Madaraka katika uwanja wa Tononoka, Nassir alisema kuwa sharti Jubilee iwajibike katika kuleta maendeleo kwa wananchi wote bila ubaguzi.“Sharti Jubilee iwajibike katika kutekeleza maendeleo kwa wananchi wa Pwani pasi ubaguzi,” alisema Nassir.Wakati huo huo, amewataka wanasiasa kutowagawanya wananchi kwa misingi ya dini au kabila.“Sio vizuri kuwagawanya wanachi kwa misingi ya dini ama hata vyama kwa sababu ya siasa. Sisi sote ni Wakenya,” alisema Nassir.Amewasihi wagombea wote wa kisiasa kutotumia matamshi ya chuki na uchochezi msimu huu wa kampeni na uchaguzi mkuu.