Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Chache Kaunti ya ksii Richard Tong’I amesema kila mwananchi ana uhuru wa kuishi mahala popote humu nchini.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Alizungumza haya siku ya Jumanne katika eneo bunge lake.

Aidha, aliomba serikali kuu kuhakikishia wakenya wote usalama wao na kuimarisha usalama  kila sehemu humu chini ili wananchi waziwe wanaishi chini ya uoga mkali wa kushambuliwa na magaidi.

“Killa mwanchi ana haki na uhuru wa kuishi popote iwe ni eneo la kisii iwe eneo la kaskazini au mashariki sharti serikali iwajibike kwa usalama kwa kila mkenya,” alisema Tong’i.

Mbunge huyo alisema familia nyingi zilizoathirika na mashambulizi ya Garisa ni maskini kwa kiwango cha juu na kusema familia hizo zilizowapoteza wezao umaskini uliongezeka mara dufu.

Kwa upande mwingine wakaazi wa eneo bunge hilo, walifuhia matamshi ya mbunge huyo huku wakimwomba kuyafanya yote yale ameyasema dhidi yao ili iziwe ni mambo ya ugongo.

“Tumefurahishwa na mbunge wetu vile amesema kuwa familia abazo ziliathirika sharti zifadhiliwe, juzi alisema hataunga mkono mambo ya ndoa ya jinsia moja iliyokubaliwa na mahakama na kusema atayakana hayo bungeni, tunaona mbunge wetu anajali maisha ya wakenya,” alisema Margret Nyambane mkaazi.