Mbunge wa Mugirango Kusini Manson Nyamweya ameulaumu uongozi wa Kaunti ya Kisii kwa kutoharakisha ujenzi ulioahidiwa wa kujenga kiwanda cha kuchonga mawe ya vinyago maarufu soapstone factory katika eneo Bunge hilo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea siku ya Jumapili mjini Kisii, Mbunge Nyamweya amejitetea kuhusiana na kuchelewa kwa kujengwa kwa kiwanda hicho akisema kuwa jukumu la kujenga kiwanda hicho ni la uongozi wa Kaunti huku akidai kuwa Gavana James Ongwae anastahili kuwajibikia ukuaji wa kiuchumi kwa kuhakikisha wananchi wanafaidi matunda ya ugatuzi kwa kujengewa viwanda ili wapate kazi na kujikimu kimaisha.

"Gavana James Ongwae sharti awajengee kiwanda hasa wakaazi wa Mugirango Kusini kama alivyowaahidi wakati wa kampeni yake ya kuwania ugavana," alihoji Nyamweya.

Nyamweya ambaye ametangaza kuwania ugavana wa Kaunti ya Kisii katika uchaguzi mkuu ujao wa 2017, amekuwa mwiba kwa na mkosoaji mkubwa wa Gavana Ongwae na uongozi wake katika kwenye siku za hivi karibuni huku akisema kuwa ataleta mabadiliko kwa kujenga viwanda ambavyo Kaunti iliahidi na imefeli kutimiza yote waliwaambia wakaazi wa Kisii.

Mbunge huyo hata amewahakikishia wakaazi wa eneo lake la ubunge kuwa atatimiza ahadi zake zote za kujenga barabara na shule vile vile atawafadhili watoto wote walio na mahitaji ya karo kwenye Vyuo ambapo aliwaomba wanafunzi kuwasiliana na ofisi yake ya CDF ili kusaidiwa.