Mbunge wa eneo bunge la Borabu Ben Momanyi amesema kwamba ataendelea kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo bunge lake ili kuinua viwango vya maisha katika eneo hilo.
Akihutubu kwenye shule ya upili ya Nyabikomu siku ya Ijumaa, Momanyi alisema kuwa agenda yake kuu ni kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye eneo bunge lake.
"Mliponipigia kura kama mbunge wenu mlinipa wajibu wa kuwafanyia kazi, na ndio maana ninazidi kuimarisha sekta ya miundomisingi katika eneo hili na hata pia kufadhili miradi ya shule mbalimbali," alisema Momanyi.
Momanyi aidha aliongeza kuahidi usimamizi wa shule hiyo kuwa atawapokeza hundi ya shillingi elfu mia 500 chini ya mwezi mmoja ujao ili kusaidia kufadhili ujenzi wa chumba cha maakuli kwa wanafunzi wa shule hiyo.
"Napenda kuipa miradi ya maendeleo kipau mbele, na ndio sababu kabla ya mwezi huu kukamilika niwape hundi ya nusu millioni ili kufadhili mradi wa ujenzi wa chumba cha maakuli kwa wanafunzi," aliongezea Mong'are.