Wahudumu wa bodaboda mjini Gilgil, Nakuru wamtaka mbuge wao Stanley Mathenge ashugulikie miradi ya barabara mjini humo ili kuimarisha sekta ya uchukuzi.
Wakiongea na mwandishi huyu Ijumaa hii mjini humo, wahudumu hao walisema barabara nyingi zinazounganisha mji huo ziko katika hali mbaya na zinahitaji kushugulikiwa kwa haraka.
Wakitaja barabara ya Anti Stock Theft kama iliokuwa katika hali mbaya zaidi, walimwomba mbuge huyo kuirekebisha.
Walimshtumu mbuge huyo kwa kuwasahau, licha ya wao kujitokeza na kumpigia kura mnamo mwaka 2013.
Alex Waweru, mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda mjini humo alisema barabara mbovu zinaendelea kuwaletea hasara kubwa kwenye sekta ya uchukuzi.
Waweru alisema wanatumia pesa karibu zote wanazopata kutengeza pikipiki zao.
"Tungekua tunapata pesa ya kutosha, lakini kwa sababu ya barabara mbovu tunatumia pesa nyingi kutengeza pikipiki, hivyo basi kufanya maisha yetu kuwa ngumu sana," alisema Waweru.
Aidha, wahudumu hao walimtaka mbuge huyo kuweka taa mjini humo ili kuimarisha usalama na pia kufungua miradi sehemu hiyo ambayo itafaidi vijana, wanawake na walemavu.