Mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire amejitokeza kumshtumu vikali mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Isaac Hassan, baada ya kudinda kungatuka afisini mbele ya kamati ya masuala haki na kisheria kwenye bunge la kitaifa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kwenye mahojiano kwa njia ya simu siku ya Jumanne, Bosire alisema kuwa yafaa makamishna wa tume hiyo wangatuke mamlakani kwa maana idadi kubwa ya wakenya wamekosa imani nao.

"Inakuwaje kwamba mwenyekiti wa IEBC Isaac Hassan anaweza kataa kwamba kamwe makamishna wa tume hiyo hawawezi ondoka afisini hata baada ya kamati ya bunge kuahidi kwamba wangelipwa pesa zao zote huku ikizingatiwa wakenya wamepoteza imani nao." aliuliza Bosire. 

Bosire aidha aliongeza kwa kusema kuwa muungano wa CORD uko tayari kufanya mazungumzo ya pamoja na serikali ya Jubilee ili kusuluhisha tofauti za usimamizi wa tume ya IEBC. 

"Muungano wa CORD upo tayari kufanya majadiliano na viongozi wa serikali ya Jubilee kuhusiana na tume ya IEBC kwa maana tungependa kushiriki uchaguzi wa huru na haki mwakani," aliongezea Bosire.