Mwakilishi wa akina mama katika kaunti ya Kwale, Zuleikha Hassan Juma ameendeleza uchunguzi wake kufuatia kifo cha Subira Hamisi.
Mwanamke huyo wa miaka 34, alifariki katika hali ya utata nje ya zahanati ya Gombato wiki jana.
Hiyo jana, Jumatatu, Zuleikha aliitembelea familia ya marehemu kuchunguza kama kufariki kwake kulikuwa kwa sababu ya wahudumu kuzembea kazi yao au la.
Aliongea na familia yake, mhudumu wa zahanati, askari aliyewazuia kuingia katika zahanati hiyo pamoja na Waziri wa Afya wa kaunti ya Kwale bwana Francis Gwama.
Mwakilishi huyo aligundua yafuatayo:
1. Mgonjwa aliwasili baada ya zahanati hiyo baada kuwa ishafungwa saa kumi na nusu.
2. Alipofika kwa zahanati kulikuwa hakuna muhudumu.
3. Alifika nje ya zahanati akiwa yu hali mahututi na kufia hapo nje.
4. Hata baada ya kuwafikia askari hakuwafungulia gate waingie kwa sababu anasema alikuwa anaogopea kuingiza watu bila ruhusa baada ya masaa ya kazi.
Zuleikha aidha, alitoa maoni yafuatayo:
1. Huenda hata kama zahanati ingelikuwa wazi, Subira angelifariki hivyo hivyo kwa sababu tayari alikua katika hali mbaya.
2. Iwapo kungekuwa na muhudumu hapo, pengine mtoto alie tumboni angeweza kusalimika.
3. Askari angewacha mgonjwa aingie ndani awekwe pahali pazuri badali ya kumuacha chini kwenye mchanga.
Kufuatia mkutano na Waziri wa Afya wa kaunti, walikubaliana kuwa:
1. Waziri wa afya aliamuru mmoja wa wahudumu walio hapo kuishi ndani ya boma hilo ili kuepuka hali ambayo zahanati haina mhudumu wakati wowote.
2. Walikubaliana na waziri kuwa watashirikiana kutoa mafunzo kwa wafanyikazi wa sekta ya afya katika kaunti ya Kwale ili wawe na muamala mzuri na wanaofuata huduma hapo. Ili kusiwe na malalamishi kama haya siku zijazo.
3. Askari wa zahanati hiyo amepewa onyo ya kuwa hata kama hakukuwa na muhudumu angewacha mgonjwa aingie ndani awekwe pahali pazuri huku familia yake ikitafuta njia mbadala ya kuwasaidia.