Mbunge wa Lamu Magharibi Julius Ndegwa akiwa mahakamani hapo awali. Picha/ the-star.co.ke

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa Lamu Magharibi Julius Ndegwa amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya kuwa na pesa bandia.

Ndegwa anadaiwa kuhamisha shilingi laki tisa pesa bandia kutoka kwa benki ya Equity hadi benki ya Gulf Africa kwa hisani ya Sheihk Mohammed Abdulkhadir katika eneo la Mombasa mnamo Disemba 30, 2014.Aidha, anakabiliwa na mashtaka mengine tisa ya kutengeneza stakabadhi bandia na kujipatia ardhi katika eneo la Magogoni, Kaunti ya Lamu.Hakimu Julius Nang’ea wa Mahakama ya Mombasa alimuachilia mbunge huyo kwa dahamana ya shilingi laki tano.Ikumbukwe kuwa Ndegwa pia anakabiliwa na shtaka la kutumia vibaya fedha za hazina ya ustawishaji wa maeneo bunge.Kesi hiyo itasikizwa hapo kesho (Ijumaa).