Mbunge wa Molo Jacob Macharia ameahidi kukarabati shule za msingi kwenye eneo bunge hilo ili kuinua hali yake.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea Alhamisi katika shule ya msingi ya Elburgon, Macharia alisema atahakikisha shule za msingi zimepata sura mpya.

“Nashukuru wote waliochangia katika kutoa fedha za kukarabati shule hii. Mradi huu utahakikisha kuwa shule zote za msingi Molo zimepata sura mpya,” Macharia alisema.

Wakati huo huo mbunge huyo aliendelea na shughuli ya kutoa basari katika shule mbali mbali ili kuwafaidi watoto kutoka familia maskini. Baadhi ya shule ambazo zilifaidika leo ni ile ya Elburgon DEB ambayo ilipewa cheki ya msaada wa kielimu kutoka afisi ya rais.