Mbunge wa Molo Jacob Macharia ameteta kuhusu idadi ndogo ya watu waliojitokeza na kujisajili kama wapi kura.
Akiongea kwenye Ukumbi wa Molo stadium siku ya Jumapili, Macharia alisema inasikitisha kuwa wakaazi wa Molo hawajajitokeza kujisajili kama wapiga kura.
Aliwataka wakaazi ambao hawajajisajili wahakikishe wametenga muda na kujisali.
“Inasikitisha hapa kwetu watu hawajajisajili kama wapigakura, ni idadi ya chini sana ambayo imejisajili,” Macharia alisema.
Mbunge huyo alikuwa ameandamana na viongozi waengine akiwemo aliyekuwa mbunge wa Molo John Njenga Mungai, MCAs Michael Wang’ombe pamoja na Beatrice Nyawira.