Baadhi ya wabunge wa Cord wameikosao ziara ya Raisi wa Uganda Yoweri Museveni humu nchini.
Akizungumza siku ya Jumanne jijini Mombasa, Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir, alisema kuwa ziara hiyo haikuwa na manufaa yoyote ikizingatiwa Museveni na Rais Uhuru Kenyatta, hawakujadiliana kuhusa mzozo ambao umekua kwa muda sasa wa kisiwa cha Migingo, ambacho nchi zote mbili zinadai kumiliki.
Nassir aliongeza kuwa swala la Migingo linawakera viongozi wengi ikizingatiwa kisiwa hicho hakijulikani kinamilikiwa na taifa gani.
Museveni alikutana na Raisi Uhuru Kenyatta siku ya Jumatatu jijini Nairobi kujadili ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kati ya nchi hizo mbili.