Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amemtaka kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Adan Duale kukoma kuingilia majukumu ya tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa barabara tatu katika eneo bunge la Mvita, Nassir amemtaka Nduale kuiacha tume hiyo kushuhulikia majukumu yake kwa mujibu wa katiba na kwamba hana haki kisheria kuingilia kazi ya IEBC.
Hatua hii inajiri baada ya Adan Nduale kusema kuwa sahihi za kampeni ya OKOA Kenya ni feki na kuitaka tume hiyo kutoshuhulikia swala hilo.
Aidha kwenye uzinduzi wa barabara hizo Nassir amesema kuwa zitainua kiwango cha uchumi wa eneo bunge lake huku akitaja kuwa itakuwa afueni kwa wafanyabiashara wakati wa kusafirisha bidhaa zao kuenda na kutoka sokoni.
Barabara hizo zimezinduliwa katika eno la Redstar, Musa A na Musa B.