Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nasir ameyataka mashirika mbali mbali kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia walemavu eneo la Mombasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza baada ya kula chakula cha jioni na jamii hiyo ya walemavu katika ukumbi wa Fort Jesus, Nasir alisema walemavu pia wana umuhimu mkubwa katika jamii, hivyo hakuna haja ya kuwabagua miongoni mwa jamii.

Siku ya Jumamosi, Nassir alisema kuwa walemavu wengi wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa za kiuchumi.

“Walemavu wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa haraka, hawana uwezo kwani wamesaulika pakubwa,” alisema Nassir.

Aidha, amezitaka serikali za kaunti na serikali kuu kuwahusisha walemavu katika miradi mbali mbali.