Mbunge wa Mvita Abduswamad Nassir amesema kuwa atawania kiti cha ugavana katika Kaunti ya Mombasa kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.
Akizungumza siku ya Alhamisi alipokuwa katika ziara ya eneo la Majengo, mbunge huyo alisema kuwa atamuunga mkono Gavana wa sasa Hassan Joho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 kabla ya kujirusha uwanjani mwaka wa 2022.
“Nitawania kiti cha ugavana katika Kaunti ya Mombasa mwaka 2022 ili kuendeleza kazi nzuri ambayo Gavana Joho atakuwa amefanya katika miaka ya uongozi wake,” alisema Bw Nassir.